Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za maisha (diaries), visa na matukio na yale unayopenda kuchangia na wenzako (mijadala), maneno ya hekima, kusaidiana na pia kutoa dukuduku lako (kilio chako). Soma na uchangie chochote kwa kutoa maoni (comments) yako, au tutumie kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA

TUNAKARIBISHA MATANGAZO YA BIASHARA HAPA

Friday, June 1, 2012

Hujafa hujaumbika-46 hitimisho-4




Mtoto wa familia ya kidocta, alizitoa zile pica kwenye bahasha, na kuanza kuitizama moja moja, na kila aliyoangalia alitamani kuichana au kuitia moto, lakini asingeliweza kutimiza hilo alilopanga kufanya, akaendelea kuzitizama na majina ya huyo mwanamke alieyepo kwenye picha na nyuma ya picha kuna maelezo wapi akaishi.

Alizitizama zile picha kila moja kwa wakati wake, na kujaribu kuvuta kumbukumbu , kama kweli aliwahi kukutana na hawo wanawake, lakini hakuweza kumgundua hata mmoja, akainuka na kwenda kusimama kwenye dirisha aliangalia nje sehemu ambayo mume wake anaweka gari lake, kulikuwa hakuna gari, na inaonyesha kama hapajatumika kwa muda mrefu.

Alikumbuka jinsi walivyopigana majuzi, na ikabidi mume wake huyo ahamie chumba cha wageni, na mara kwa mara alikuwa akiamuka kuhakikisha kuwa hapitilizi na kwenda chumba cha binti yake wa kulea, alishaamua kumlinda kwa nguvu zake zote, …

‘Huyu mtu atakuwa hajalala ndani, sijui atakuwa kalala wapi, nikipagundua, huyo mwanamke wake nitamtoa nyongo….anachezea mali ya mtoto wa mama docta..ngoja leo akija , nitamshika mguu kwa mguu hadi kwa huyo mwanamke wake….’akasema lakini alipowaza jambo, akaona ngoja kwanzaatafakari kazii aliyopanga kuifanya,…kamaitafanikiwa,ataweza kulikomesha hili, sio kwa mume wake tu, hata kwa waume wa wengine ambao wana tabia kama hiyo….

Akakumbuka mawasiliano na mama yake ambaye alimpigia simu akitaka kuomba ushauri, maana kazi anayotaka kuifanya inahitaji mtu mzoefu,…anakumbuka alishawahi kushauriiwa na mama yake aanzishe kliniki yake na iwe kama tawi,…..lakini akakataa, sasa wazo la kuianzisha likamjia, lakini alitaka aianzishe kwa namna tofauti….

‘Bintiyangu unaniangusha, mimi ni docta ambaye nawasaidia walio na matatizo ya ndoa zao, niwafunda wake za watu ili ndoa zao ziwe na furaha, leo nashangaa  kusikia kuwa wewe hupatani na mume wako, unajau unaniabisha….’akasikia sauti ya mama yake akiongea kwenye ubongo wake.

‘Ina maana mimi ndio nimeshindwa kutimiza wajibu wangu au ni mwenzangu, kwani wapi nimeshindwa kutimiza wajibu wangu, najitahidi sana pamoja na majukumu yangu ya kazi,lakini bado natimiza kila jambo linalonistahili mimi kama mke wa mtu….’akajikuta akijiuliza.

‘Hebu niambie tatizo liko wapi, binti yangu…?’akasikia sauti hiyo ikimuuliza.

‘Mama , mimi silioni tatizo, …na kukupigia simu, sio kwamba nimeshindwa, sijashindwa, ila jibu la swali lako kuwa tatizolipowapi, ni kwamba,nimejribu hata mimi mwenyewe kufanya utafiti ili nijue tatizo lipo wapi nimeshidwa, nimejaribu kumweka mwenzangu karibu, kumhoji, kumdadisi, ili niweze  kujua nini anataka,lakini nimeshindwa..’akajitetea

‘Ulipomuuliza nini anataka alisema nini?’ akaulizwa.

‘Anasema yeye kama mwanaume hastahili kuchungwa, anachotaka ni yeye kufanya yake anayoyaona yeye kama mwanaume anastahili kufanya, hataki aulizwe wapi katoka na kwanini kachelewa kurudi,..na kila kihitaji lolote, hataki kusikia nimechoka,sijisikii….mama,inakera…’akasema

‘Ni hayo tu binti yangu, na mambo mengine ya kindoa unamtimizia ipasavyo…?’ akaulizwa.

‘Yote najaribu kumtimizia, lakini wakati mwingine mama unakuwa umechoka,mwenzangu hashibi,…hashibi kabisaaah, uelewe mama mimi ni mfanyakazi, na unavyojua kazi zetu, unatembea ndani ya hospitalini,nenda rudi, panda shuka, ukipima huo umbali uliotembea humohospitalini,ni kama umetembea maili nyingi sana,…..achilia mbali kusemeshana na watu, kushughulikia hawo wagonjwa, unajikuta ukirudi nyumbani umechoka, na ukirudi nyumbani majukumu yanakungoja,…..’akajitetea.

‘Niliwashauri mtafute mfanyakazi wa nyumbani mlifikia wapi….?’ Akauliza.

‘Mama hilo sitalirudia tena kwa sasa, unajua yule binti wa watu nilyekuambia nilimchukua atusaidiekazi, alichofanyiwa na huyu mume, ni aibu hata kuongea, achilia mbali huyo mfanyakazi yule ndugu yetu niliyemchukua toka kule kijijini, naye unajua nini kilichomkimbiza toka hapa, watu wanazani kuwa labda mimi ni mkali siwezi kuishi na wafanyakzi wa nyumbani, lakini sivyo hivyo, nimeficha siri za mumewangu tu,….’akatulia na kwikwi za kilio zikamtawala.

‘Kwahiyo huna mfanyakazi tena hapo nyumbani kwako,anayekusaidia majukumu mengi ya usafi,kufua …..?’ akaulizwa.

‘Kazi ndogo ndogo ananisaidia yule binti yetu,yule binti ,ambaye nilichukua kijijini akiwa anakula majalalani, tuaamua tumchukue tumlee kama mtoto wetu…kawa bint mkubwa, nakwa vile kaanza kupendeza, basi mume wangu keshaanza kumwangalia kwa macho ya tamaa…..’akasema

What….huyo sio sawa na mtoto wenu, nakumbuka mliniambia kuwa huyo mtamfanya kama sehemu ya familia yenu,,….sasa iweje leo, mimi huyo simuiti kama mfanyakazi wenu wa nyumbani,huyo ni mtoto wenu….. unasema mumeo anaanza kutoa mate kwa ajili yake….its too much,….mwanagu njoo nikufunde, kuna tatizo hapo, kuna kitu umeshindwa kwa huyo mumeo,…..njooo haraka….’akasema mama kwa hasira

‘Mama, sijashindwa…mama, inaniuma sana, ukisema mimi nimeshindwa siwei kukuelewa,labda kwa vile humjui huyu mume wangu, nimeshindwa nini mimi mama, huyu mume anataka nini cha zaidi…lakini hata hivyo mama mbona ….’akaanza kulia tena….

‘Sasa ndio unalia,…usiniangushe sitaki wanangu muwe legelege, pambana kiume….mmh,kikike, wewe ni mwaanmke,bwana,wewe ndiye muhusika mkuu wa ndani ya nyumba yako, ukishindwa kuilea familia yako,akiwemo mume wako, utachekwa,….nasikitika sanakuona unalia, kulia huko kunaonyesha kuwa mume kakushinda,kama vipi njoo ukae na mimi wiki mojatu,ukirudi huko utanimbia,…ni aibu kusikia kuwa mmoja wa binti yangu ana matatizo kama hayo….’mama akamwambia.

‘Wala sihitaji kuja huko mama,nimeshajua nini la kufanya, yeye si anajifanya kidume,ngoja nitapambana naye kumuonyesha kuwa mimi ni mwmanake wa shoka….mtoto wa mama Docta…’akasema huku akikunja ngumi.

‘Nataka kusikia hivyo, sitaki watoto wangu muwe laini laini, pambana na familia yako, jiulize wapi nimekosa, angali nini mume anataka, na kwanini awatake hata mabinti wa nyumbani, ndugu zako….ina maana wewe hutatembelewa na ndugu wa kike,….huyo hujamshibisha, hujamjulia nini anataka…na miaka imepita hamjajaliwa mtoto, hilo sio kosa lenu, ila jitahidini kupimwa, muangalia huenda kuna tatizo jingine.

‘Binti yangu ndoa sio lelemama,ndoasio kufika kwa mume kama mbia,kama mshirika wa biashara, ndoa ni jukumu lako, ukifika ujue wewe ndiwe mlezi, wewe ndiye kila kitu kuhusu malezi, mume, ni mume tu, yeye anahitaji malezi yako pia. Mume ni kama mwenyekiti, wewe ni katibu, hebu angalia kazi za katibu na mwenyekiti, ni mfano dogo tu, ila ni zadi ya hapo….

‘Mama nimekuelewa, hilo niachie nimeshajua nini cha kufanya, nitapambana naye hadi nionemwisho wake, sihitaji msaada wamtu….’akasema akiwa kakunja uso kwahasira.

‘Pambana naye, usishindwe majukumu yako ya nyumbani, ukishindwa wenzako watakucheka, na wakijua udhaifu wako, watamchukua mume wako kijumla….chunguza hawo wanaomvuti mume wako wana nini cha zaidi, ukijua fanay zaidi yao….sioni kwaniniushindwe….’mama yake akasema.

‘Nitapambana naye,…tutaona…na nitajua nini walicho nacho cha ziaidi,na mimi nitawaonyesha  kuwa najua zaidi….utasikia siku yeke….’akasema.

*******

‘Binti Maringo, Kimwali, Kimwana,…..mama Docta…’aliposoma hilo jina akashituka, anachojua yeye mama docta ni jina ambalo huitwa mama yake, na ndugu yake pacha,….anakumbuka kuwa hata yeye alipenda kulitumia hilo jina alipokuja mara ya kwanza, alikuwa kijiita hivyo, lakini hilo jina halikudumu sana….hakulipenda.

‘Mama Docta ni nani huyu,….?’ Akajiuliza, akachukua simu na kumpigia mtu wake ambaye kampa kazi hiyo ya kufuatilia nyendo za mume wake.

‘Hebu niambie huyu mama docta ni nani?’ akauliza.

‘Ni dakitari mmoja, ndivyo anavyoitwa, ….’akasema huyo mtu wake.

‘Yeye mara kwa mara wanakutana wapi na mume wangu?’ akauliza.

‘Mhh,hawana sehemu maalumu, mume wako mara nyingi ndiye anatemfuata, hasa baada ya kukosana Kimwana, kimwana alikuwa rafiki yake wa mara kwa mara, kila akitoka hapo kwako anakwenda huko kwa Kimwana, lakini baadaye akakutana na huyu mama Docta, kipindi anaumwa, naonahap ndipo alipokolea,….’akasikia maneno hayo na hasira zikampanda.

‘Kwahiyo analala huko huko,au?’ akauliza.

‘Sijawahi kuona akienda kulala huko huko,maana huyu mamadocta ni mkali sana kwa wanaume, hapendi wanaume…’akasema.

‘Kama hapendi wanaume,mbona anampenda mume wangu?’ akauliza.

‘Mume wako ndiye anayemtaka…kiukweli inavyoonekana ndivyo hivyo,kuwa mumeo ndiye kazimia kwa huyo docta, huyo docta ni mrembo kweli, na kinachowafanya wanaume wengi wazimie kwake, ni huko kutokupenda wanaume,…unavyomjua mume wako, alivyo akadai yeye hatongozi mke akashindwa,.. wakati mwingine unaona kabisa, mume wako akihangaika kuongea na huyo mama docta, lakini huyo mama docta anaonekana kukataa….’akasema huyo mtu wake.

‘Lakini kwenye hii picha wanaonekana kabisa wakibusiana…na inanichefua kweli hii picha…nikikutana na huyu mwanamke ataniona kuwa mimi ni nani...’akasema.

‘Kwenye hiyo picha hapo, alikuwa akilizimisha hilo busu, niliwakuta wakati wanapata chakula cha mchana, na kama kawaida mume lazima apate kichngamsha kichwa, nafikiri baada ya kukolea akaona afanye hicho unachokiona hapo, mwenzake alikuwa hakubali…., akamshitukizia kumbusu, mumeo kweli naye hajatulia…..lakini kwanini anafanya hivyo humshibishi nini….?’ Akauliza huyo mtu wake.

‘Mimi sijakupa kazi ya kunichunguza mimi, kuwa nafanya nini na mume wangu, unanisikia lakini,, kazi yako ni hiyo kumchunguza mume wangu anafanya nini na hawo wanawake, usianzekunichefua, maana nyie wanaumelenu moja,….sasa nataka kazi moja kutoka kwako…..njoo hapa kesho tutapangane jinsi ya kuifanya,….’akasema na kukata simu.

NB: Ni kazi gani hiyo, tuendelee kuwepo. Samahani kwa kuchelewesha kuweka sehemu hii, nilichelewa kufika kijiweni, na bosi akaingia mapema, ikabidi nitulie kwanza. Hata hivyo sijaweza hata kuipitia, nimeiandika kwa haraka, kama kuna makosa tusadieni kusahihisha. Tupo pamoja
WAZO LA LEO: Ukitenda jambo kwa mwenzako, au kusema neno kwa mwenzako, kwanza jiulize je mimi nikitendewa hivyo, au kuambiwa hivyo nitafurahi, isiwe mkuki kwa nguruwe tu, kwa binadamu uwe mchungu.

Ni mimi: emu-three

Thursday, May 31, 2012

Hujafa hujaumbika-45 hitmisho-3




Tukiendelea pale tulipoachia kuhusu kisa cha binti wa kijijini,

Binti huyu aliyeathiriwa na kutendwa, kutokana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa ya utotoni, ndoa iliyokuwa baina ya Msomali na huyo binti na mshahidi walikuwa Mungu muumba Wa viumbe na malaika wake. Ilikuwa ni ndoa ua utoto, lakini….Haya tuendelee na kisa hiki;

                                                                   %%%%%%%%

‘Hivi kweli niwaulize, kuna ndoa ya utotoni ambayo inaswihi, mimi najua ili ndoa ikubalike ni lazima watu wawe na umri unaojulikana kuwa hawa wamepevuka kiakili, na pia ili iwe ni ndoa ni lazima kuwe na wafungishaji ndoa na pia wawepo mashahidi, …sasa mnapotoka kunitupia lawama mimi kuwa eti ndiye niliyesababisha hadi huyo binti kuathirika kisaikolojia, nashindwa kuelewa,…ikizingatia kuwa wewe ni mwanasheria unayajua hayo yote kuliko mimi…’nikajitetea pale nilipoona wakili mwanadada akitulia.

‘Ndio hilo unaloongea ni sawa, sijakataa,na wala sijasema ndoa hiyo inakubalika kisheria, ila mwenzko aliichukulia kuwa ni ndoa kamili, najua kuwa haikuwa na yale mambo muhimu yanayohitajika kuitwa ndoa, na kwa ujumla haiswihi kuitwa ndoa, ni michezo ya utotoni, lakini nikuulize wewe wakati mnaifunga ile ndoa ulikuwa na dhamira ya kweli kuwa unaoa, au mlifanya kama mchezo tu, ulikuwa ukimpenda kiukweli au ulikumwa mchzo wa kitoto…?’

‘Niseme kiukweli, wakati tunaifunga ile ndoa, nilikuwa na dhamira ya kiukweli kuwa naoa, na baada ya tukio lile, nilimuona kama ni sehemu ya mwili wangu, na hata leo nahisi hivyo, lakini ujana na damu yangu kuchemka, nikasalitika, na niseme …yakatokea yaliyotokea, …..’nikajitetea.

‘Sasa unaona hilo, mwenzako ilikuwa zaidii ya hilo, alijizuia kwa kila hali akijua kuwa ana mume,….toka siku ile,…na siku ile alipokufumania akajua umehini ndoa, na akaathirika kiukweli, na ndio chanzo cha matatizo yake ya kiafya hadi leo hii..

‘Una maana gani kusema hadi leo hii, kwani una habari zake, kuwa yupo wapi, …?’ nikajikuta nauliza

‘Usiwe na pupa kwani sio wewe peke yake unayetaka kujua hayo , nataak kila mtu aelewe hatua kwa hatua, ili mwisho wa siku muone athari zinazotokana na kusalitiwa katika `kupendana’husuani kwenye ndoa.Tujue kuwa sio wote wenye uthabiti wa kuvumilia matatizo, ndio maana unaona wengine wakipata matatizo kidogo tu wanaathirika na wengine wanadunda, hata iweje, ni hula na maumbile ya kibinadamu.

Tukirejea pale tulipoishia kuwa binti huyu kila akipata mchumba, ndoa hiyo inakuwa haifungiki, ama kunatokea ajali au matatizo ambayo yanaisimamisha hiyo ndoa.Na haikutoka mara moja, ni zaidi ya mara tatu,….Hutaamini hayo, lakini yalitokea kwa huyu binti,na ukianglian sana inapotokea hivyo, anayeathirika sana akilini ni nani….mara nyingi anakuwa ni mwanamke…hayo ni maumbile

Kwa mtizamo huo na maneno ya yule mtaalamu wa mwanzo wa sili, na histora ya matatizo yake ikaonekanahivyo,  kwa hawa wazazi na pia kwa jamii na wanajamii waliobahatika kulijua hilo tatizo kuwa kweli huyo binti anatawaliwa na huyo jinni mahaba. Hapa muwe makini,muone jinsi gani hawa wataalamu wanavyojua kuzichota hisia za watu kisaikojia, sio kwamba na wapinga, lakini sio kweli kuwa wote wapo sahihi kwa yale wanayoyasema.

Wazazi kusikia hivyo,wakaamua kulifungia kazi hilo tatizo, kwa wataalamu ,huku na kule, na kila wapofika wimbo ni huo huo, ….mtoto wenu ana meshetani, anatawaliwa na jinni, ….je ni nani hataacha kuamini hayo, hasa kwa wazazi wa binti,.., zaidi ya wataalmu sitawote wanasema kitu hicho hicho,wakajua ni kweli, sasa wanatakiwa kuliondoa hilo shetani,..wafanyeje.

Kwanza walifuata hayo waliyoambiwa na wataalamu wa kiasili , dawa za kufukiza, sijui maji ya baharini, kuku mwekundu,…vitu vingi tu, ….lakini wapiiiii….tatizo likawa linajirudia ingawaje si mara kwa mara ila ni pale tu inapofikia huyu mwanadada kapata mchumba au rafiki wa kiume. 

Basi wazazi wakaona hilo sasa tuwaendee watu wa dini, wakawatafuta waombezi wa kidini, wakaombewa, na wao hawakuchagua dini gani, kila wanayemuona ni mtu aliyesomea dini na anajua jinsi gani ya kumuombea mgonjwa aliyeathirika na mshetani, wanamuomba atoe msaada huo.,….imani ni kitu cha pekee yake na mungu hamtupi mja wake, baada ya maombezi hayo, hali  ilionekana kuwa imetulia, lakini sasa likazuka tatizo jingine.

Kila mwanaume aliyakutana na huyo binti, akampenda, wakakubaliana na hata kufikia hatu ya kujimbulisha kama wachumba, mwanaume huyo akirudi nyumbani kwao kutoa taarifa, akiulizwa na mwanamke gani, akamtaja huyo mwanamke, naambiwa wewe, unataka kufa na jinni mahaba, shauri lako, angalai wenzako, mtoto wa nani na anni wako wapi sasa,…achana naye , wanawake wapo wengi, katafute mwanamke mwingine usiingie kwenye balaa….

Basi ikawa mkosi kwa binti huyu, wanaume wengi, wakawa wanamuogopa, na hali hii ya kunyanyapaliwa, ikamuathiri zaidi, akajiona ni mwanamke wa mikosi,  kuwa yeye sio mtu wa kawaida,..na kuanzia hapo, akawa hataki urafiki na wanaume, chuki ikajijenga akilini,  na hasira kwa wanaume  ikazidi.

Chuki hiyo ilikuwa kwa wanaume wote,na wakati huo, akili yake haikuwa ikitambua kuwa chanzo cha yote hayo ni athari iliyojijenga akiwa msichana mdogo, kuwa yeye bado nafsi yake ipo kwenye pendo la mwanzo, pendo lake na mvulana wa utotoni na ujanani ambaye ndiye aliyeathiri akili na nafsi yake….

‘Mume wangu, mimi naona tuhame kabisa hapa, maana kwanza biashara haiendi vyema, pili, binti yetu anaathirika kisaikolojia,turudi kwetu, ama kijijini au mahali pengine , ambapo watu hawajui lolote kuhusu binti yetu….naona anateseka sana’akasema mke.

‘Hilo wazo lako sio baya, hata mimi nilishaliwaza hilo, sio kuliwaza tu, bali nilishawasiliana na ndugu yangu anayeishi huko Dar, ana jengo lake lipo sehemu nzuri ya kibiashara, tutahamisha baadhi ya shughuli zetu na nyingine zitaendelea kuwepo hapa, …bado mambo machche ya kisheria kama leseni lakini hilo litakamilika hivi karibuni….’akasema mume.

‘Je na huyu binti yetu kuhusu kazi yake ambayo keshaianza hapa itakuwaje?’ akauliza mke.

‘Hilo nalo nimeshalifanyia kazi, kuna nafasi nyingi zakazi za madakitari huko Dar, na ni swala la yeye kupeleka vyeti vyake hukoo na barua ya maombi, atapata kazi hilo halina shida…sisi tuanze tu kujiandaa.
Na binti yao akafahamishwa, na yeye hakuwa na pingamizi, na safari ya kuja Dar ikakamilika


Sasa turejee kwa familia ya madakitari, familia ambayo baba, mama na watoto wote walibobea kwenye fani hii ya udakitari, na hata kufikia hatua ya kuanzisha kliniki yao, na sio kliniki tu,bali kikawa chuo cha kufundisha madaktari au watu  waliotaka kujua maswala ya kimaumbile,hulka na hisia hasa katika maswala mazima ya mahusiano, huku kwetu tunaita kufundwa, wao waliyaweka kitaalamu zaidi.

‘Unataka kuoa au kuolewa, una matatizo ya kindoa, una matatizo ya uzazi, una matatizo ya kifamilia na mengine mengi, fika kwa kliniki ya mama Docta, …’ hilo ni moja ya tangzao lao, ukifika huko Kenya utalikuta.

‘Unasema Mama Docta,ina maana ni yule mama aliyetoroka hapa nchini…..?’ nikauliza huku nikiwa nimewaka kwa hasira.

‘Hebu nikuulize swali, huyu mama aliyetoroka hapa ana umri wa kuweza kuzaa watoto wakubwa wakuolewa…jinsi ulivyomuona wewe?’ akauliza wakili mwanadada.

‘Hapana ,…yule mimi nilishakutana naye, hana umri huo,licha ya kuwa anavaa miwani mikubwa na nywele zake ni nyingi, nafikiri ni za bandia, ..huwa kama akaficha sura wakati wote, lakini ukimwangalia kwa karibu,sio mtu mzima wa kuwa na watoto wakubwa kiasi hicho,,maana mwanamke aliyezaa mabinti waliofikia umri wakuolewa,hajifichi….’akasema mkuu.

‘Sasa… mbona hapo mnanichanganya, hebu endeelea tusikukatize…huenda nikapaat jibu…’nikasema.

‘Ndio maana nawaomba mnipe nafasi,maana mimi nimelifanyia hilo utafiti wa kina, najua kila kitu, kuhsu hawo watu, mkianza kunikatisha-katisha, nitalipua lipua na hamtaelewa vyema….’akasem wakili mwanadada.

‘Haya endelea…’nikasema huku nikajaribu kumkumbuka huyo docta mama, sikuwahi kukutana naye uso kwa uso, nilikuwa namuona kwa mbali tu….

Ukumbuke kuwa ndani ya kliniki hii, pia alipitia binti ,aliyekuwa mchumba au mke wako wa utotoni, na hapo ndipo alipopatia mafunzo  mazuri ya uzazi, hulka za kimaumbile, na ukichanganya na fani yake ya udakitari, basi akaamua kuusomea kabisa udakitari  bingwa wa matatizo ya kina mama , na kwa vile alishaanza kutibu hapo, kusaidia na hata kufundisha wengi wakawa na yeye wanamuita mama-Docta.

Kwa jinsi alivyofaulu, na kuweza kufikia kiwango cha hali ya juu, katika kliniki hiyo, au chuo hicho,wenyewe waliamua kumchukua kabisa awe mmoja wa dakitari wao, au mwalimu wa chuo hicho, lakini mara ikaja hiyo hoja ya kuhama hapo Kenya na kuja huku Dar,ikabidi asamehe kwanza hiyo nafasi, kwani hata yeye alishachoka na hali iliyopo hapo, kila mtu anamnyoshea kidole yeye, kuwa ni mke wa jinni mahaba.

Yeye mwenyewe baada ya kusoma sana na kupata mafunzo hapo, na kukutana na mama mtaalmu mwenyewe,akajijua kuwa sio mambo ya mshetani kama wanavyojua watu, lakini ni athari za kisaikolojia na hutaamini huyu mwanamama alikuja  hata kulifichua hilo, katika kumsaidia huyu binti, alichimbua historia ya huyu binti ahdi akagundua chanzo cha matatizo hayo ni nini …nakweli huyo binti akakubaliana na huyu mama kuwa kweli  chanzo cha hayo yote ni athari za yale yaliyojijenga akilini mwake akiwa mdogo,..

‘Sasa nitaondokaje na hili tatizo ,nifanyeje mama docta…?’akamuuliza huyo mama.

‘Kwani inavyoonekana bado akili yako inampenda huyo mtu, lakini kwa yale uliyoyaona na kwa jinsi ulivyokuja kuona kuwa huenda mwenzako alikuhadaa, mapenzi kwako yakaanza kuingiwa na wivu, na chuki za kutaka kulipiza kisasi, ….inawezaisiwe kwa kutumia nguvu, lakini kwa kutaka kumuonyesha yeye kuwa ni mbaya, akili ikawa inahagaika kutafuta njia,..na ikiwezekana umrudishe katika iel hali mliyokuwa nayo, akili imekuwa ikimtafuta,….mwili hautaki…kunatokea mgonganoo hapo, ‘ akasema huyo mwanamama.

‘Nakushauri kama  inawezekana jitahidi ukutanae na huyu mwanaume,au tafuta mume ambaye ataweza kuteka nfsi yako,akuoe,..mume ambaye ataweza kukusahaulisha hayo yote yaliyojijenga akilini mwako, muelewevu…..’akapata huo ushauri na kila mara alijaribu kukutana na huyu mwanamama,na kwakuw akaribu naye sana, na hata aliposema anaondoka,mama yule alimuomba sana abakie, lakini haikuwezekana.
Naomba tuwe tunawasiliana, na kama ukibadili mawazo, nitafurahi sana,na ikibidi tunaweza tukafungua tawi huko Dar, nipi mbioni kwahilo….

******

Tukija kwenye familia yetu hii ya madakitari, ukumbuke kuwa binti mmoja alijiengua ndani ya family ahiyo mapema, na kuja kufanya kazi  huku Dar, na ushawishi huo ulitokana na urafiki uliokuwepo kati ya binti huyu na mavulana toka Tanzania, ambaye walikutana huko chuoni walipokuwa wakisoma Ulaya. Ingawaje walikuwa wakisoma fani tofauti, lakini wakajikuta wakipendana…..

Na wazazi hawakuwa na pingamizi maana siku hizi watoto wakikutana popote, na wakapendana, hakuna udadisi tena wa family ahiyo ipoje, kuna matatizo gani ya kurithi, hayo wanasema kuwa yamepitwa na wakati, ….wazazi wakabariki uchumba huo, na ilipifika sehemu wazazi wanataak kukutana, ikawapeleka wazazi wa binti kusafiri hadi nyanda za ziwa. Nia na lengo ni kujua wapi huyo mvulana anatokea.

Walipofika huko, wakajikuta kumbe asili yao ni moja. Maana familia hiyo ya madakitari,asili yao ni huko huko mikoayaziwani,Tanzania, ila wazazi wao walihamia huko Kenya muda mrefu na wakazaliana huko Kenya kukawa ndio nyumbani.

Ikawa ni shangwe wenyewe walisema ng’omba karudi zizini. Basi, ndoa ikahalalishwa na kufungwa ndoa ya kifahari, baada ya ndoa bwana yeye alikuwa akifanyia kazi Dar, na ikabidi amfanyie mipango mke wake na yeye akafanyie kazi huko Dar, na hapo ndipo maisha yao yalipoanzia…

‘Mimi nataka tuwekane wazi, unakumbuka wakati tupo chuoni, kuwa mimi sitaki mambo ya kuchungwa, amri za ajabu ajabu,mimi nakuhakikishia kuwa nakupenda, na sitakusaliti kamwe, na na wewe nataka iwe hivyo hivyo, nakuomba sana, tuchunge misingi ya ndoa, na kama kuna tatizo tuambiane,mimi najua sana maisha ya ndoa kinadharia na najua mengi katika mwaswala ya mahusiano, tutasaidiana ukiwa muwazi kwangu,….’akasema mwanandoa huyu.

‘Kwani una wasiwasi gani na mimi,…mimi nakupenda, na kilichonifurahisha ni kuwa unajua mapenzi,ila mimi ni mume wako,…unatakiwa utii amri za mume wako, na sio ujiwekee mashari yako,haiji namna hiyo….unajua mila na desturi zetu zilivyo,…..mume ndiye kichwa cha familia, usiniletee mamabo ya Ulaya hapa….’akasema kiutani, lakini kumbe moyoni mwake, haikuwa ni utani.

Bwana huyu kila akikutana na wenzake, ambao walitoka pamoja huko kijijini wakawa wanamcheka kuwa katawaliwa na mke,anafugwa,wenzao wanandoa lakini wana uhuru, wanakutana kwenye mabar, wanakunywa ,wanabadilishana mawazo, …..yeye kila mra yupo nyumbani, kusaidina na mkewe kupika, wakawa wanamzihaki, na kweli kauli na maneno ya wenzake yakaanza kumteka akilini, akaona hayo maisha anayoishi na mkewe, sio sahihi,hatayaweza, akaanza kubadilika….

‘Mume wangu unatatizo gani….’akaja kuulizwa na mkewe,ambaye ni dakitari, dakitari anayejua mambo hayo, lakini wahenga walisema kinyozi hajinyoi, na penye miti hapana wajenzi. Mume akaanza kujenga dharau, mkeatakufundisha nini,mke anajua nini…

‘Mimi sina tatizo,…..kwani kuna shida gani,…?’akauliza huku akiwa kakunja uso kiaskari.

‘Naona mabadiliko,huwi karibu na mimi tena,na huo mtindo wakunywa pombe kupitliza umeuanzia wapi, hebu niambie una tatizo gani ili niweze kukusaidia….’akauliza mke.

‘Nimeshakuambia sina tatizo,….kwani wewe unataka nini,mimi ni mwanaume,natakiwa niwe huru,sio kufundikwa ndani kama mwali,…..unanielewa,…na kazi yangu ilivyo, nahitaji kuwa hivyo,..usijifanye kwavile ni dakitari unajua kila kitu,kwangu hujui kitu kuhusu ndoa….’akasema kwahasira na kuondoka,…

Mambo yakaanzia hapo…..

Ni mimi: emu-three

Wednesday, May 30, 2012

Hujafa hujaumbika-44 hitimisho-2



‘Kuna wataalamu wanasema mapenzi ya mwanzo, yana nguvu sana, ….macho na hisia za zinazomkuta mke au mume kwa mara ya kwanza, zinakuwa na nguvu sana, inakuwa kama mtu amepata kitu ambacho ni kizuri kwa mara ya kwanza, kama ujuavyo kuwa mapenzi ni jambo la kufurahisha na kupendezesha moyo, huitawala hisia ya mwanadamu, ni mambo asilia katika mwili wa mwanadamu….ni kama vile unapolamba asli kwa mara ya kwanza, utasema hakuna kitu kitamu kama asali duniani.Na hili halitawala hata hisia za kutenda tu, pia hutawala hisia za kuona na kusikia.
.
Kama unavyokumbuka Msomali, ukiwa mdogo, ulitokea kupendana na binti, jirani yako huko kijijini, yule mchumba wako wa utotoni, na unakumbuka mliwahi hata kufikia kufunga ndoa ya utotoni,…yale yalikuwa maswala ya kitoto, lakini yalijijenga ahdi mlipokuwa vijana,…naunakumbuka kipindi hicho cha uajanini, uliwahi kukufumaniwa,…ukumbuke kuwa mwenzako ule uchumba wa utotoni, hadi ujanani, ulikuwa wa kweli na ulimkaa moyoni, kwasababu alikupenda kiukweli, toka utotoni …. Hilo wewe huenda ulilichukulia kama mambo ya utotoni au sio…...

‘Sitaki useme lolote, najua ulishaniambi kuwa  bado ulikuwa unampenda, lakini upendo gani huo wa  namna hiyo, uwe na wasichana wengine, na mwenzako aweanakuangalia akijua etu unampenda,..yeye alikuwa akikuona na wasichana wengine, na mapaka siku hiyo akaja kukufumania, na kiukweli, siku ile alipokufumania, mwenzko ilimuuma sana, na sikumuuma tu, kwa maneno, yeye alikuja kuathirika kabisa kiakili, kisaikolojia, ingawaje baadaye wenzetu walikuja kulitafsri vingine,…

Siku ile aliporudi kwao akawa kama mtu aliyekumbwa na mashetani, kwani alipofika kwao alidondoka, na alipoinuka akawa anaongea lugha za ajabu, anaweweseka,….kama ungelijua kipindi kile ungelimuendea na kumuomba msamaha, huenda ingelisaidia,lakini sivyo ilivyokuwa, …na wao kamafamilia hawakuwa wanajua undani wa mahusianoo yao, na hata hivyo bado mlikuwa vijana, kama wazazi hawakujua jinsi gani binti alivyoathirika na tatizo hilo, wao walijua ni matatizo mengine kabisa.

Kwa kipindi hicho wewe ukajifanya kama hujali, kwa lile tendo la kufamaniwa, ulijiona wewe ni rijali, ni mwanaume,nahata hivyo ulisema kuwa hamkuwa mumefunga ndoa, kwahiyo hana ruhusa ya kukufuatilia maisha yako, hukuwa umeikumbuka ndoa yenu ya utotoni, kuwa mwenzako ilikuwa ni ndoa iliyokaa akilini, na aliiona kuwa ni ya kweli,…ilehali mwenzako ilimtesa, na kule kudondoka na kuweweseka, kukawa kuna mrudia mara kwa mara, wazazi hawakujua chanzo ni nini, wakahangaika kwa matibabu ya kila namna.

Baadaye waliporudi huko Kenya ambapo walikuwa na masikani yao pia, walitafuta wataalamu wa ushauri, madakitari bingwa ambao walijaribu kumsadia,lakini kiukweli haikusaidia kitu, kwasababu dakitari na dawa yake ni wewe, hakuna mwingine angeliweza kumtibia, lakini nani angelijua hilo, kwana hata huyo mgonjwa mwenyewe hakuwa na hali ya kujielezea kuwa chanzo nini, kwani hata yeye mwenyewe, hakuwa na ufahamu tena wakujua kuwa chanzo ni ile hali iliyokuwa umejijenga akilini mwake, na iliyokuja kuathirika na yale uliyomtendea wewe,,…

Binti akawa mgonjwa, mtu wa kuangaliwa na kuchungwa wakati wote maana ukimuachia anakimbia., anakimbilia wapi ,mwenyewe anadai anakwena kumtafuta mchumba wake,…..akawa anasoma kwashida, chini ya uangalizi wa karibu.

‘Huyo mchumba wake anayemtafuta ni nani…..?’wakawa wanaulizana wazazi mara kw amra bila jibu, maana wakimuuliza binti huyo mchumba ni nani, anasema  yeye hajui, na wala hakumbuki kusema kitu kamahicho, fahamu na kumbukumbu zanyuma zilikuwa hazijijengi,…zimejificha.

Waalipomuuliza mtaalamu mmoja wa mambo hayo ya mshetani, akawaambia;

‘Huyu ana jinni mahaba, na anaposema kuwa anakwenda kumtafuta mchumba wake, ni huyo jinni anamuita,….’akasema mtaalamu.

‘Sasa utamsaidieaje binti yangu, ukaliondoa hilo jinni mahaba?’ akauliza mama.

‘Anatakiwa akatibiwe baharini usiku wa manane, na kuku mwekundu, kitambaa cheusi,….’akaorozeshewa vitu vingi, ambavyo waliona wao wenyewe hawataweza kuvipata, wakatoa pesa ili huyo mganga akavitafute mwenyewe, na matibabu hayo yakafanyika, lakini haikusaidia kitu, ingelisaidiaje wakati ugonjwa huo sio kama alivyosema huyo mtaalamu, ugonjwa huo chanzo chake ni wewe….’akasema wakli mwanadadana huku akiniangalia mimi.

Walikaa sana Kenya bila kurejea nyumbani kwao, na akasoma huko, licha ya matatizo hayo ya kiafya lakini akili yake darasaniilikuwa nzuri tu akafaulu , kwenda masomo ya juu, na jinsi siku zilivyokwenda afya yake ikawa inabadilika,ila ambacho kilishindikana kuondoka ni chuki,dhidi ya wanaume.

Pale karibu yao kulikuwa na kiliniki imefunguliwa, ilikuwa kliniki ya matatizo ya akina mama, uzazi, ushauri nasaha na ndoa na mahusiano, ilianzishwa na familia moja ilikaa nje kwa muda mrefu, na waliporejea hapo 

Kenya waliamua kufungua kliniki hiyo, moja ya mambo waliyokuwa wakiyashughulikia ni maswala mazima ya ndoa na mahusiano.


Kliniki hiyo ilikuwa pia ikitoa mafunzo kwa wale wanaotaka kusomea mambo hayo, na pia ilikuwa ikitoa mafunzo kwa wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa kabla wajafunga ndoa na baadaya kufunga ndoa, hili wenzetu waliosoma wanalijua vyema, kuwa ndoa ni nusu ya maisha ya binadamu, kwahiyo inahitaji kuilewa, ni hilo limekuwa ni tatizo katika jamii, kama ni tatizo kumbe basi mtu anaweza akawekeza huko.

Familia hii ilikuwa inalijua hilo tatizo, kwani baba alikuwa dakitari bingwa wa akina mama, na mama alikuwa matroni, aliyebobea katika  maswala ya uzazi,  wakiwa huko Ulaya, walisomea kiukamilifu hiyo Nyanja na kumtafiti mwanadamu mwanaume na mwanamke jinsi alivyo, kisaikolojia ,kimaumbile na y ale yanayomkwaza husasani katika hisia za kimwili.

Familia hii ilibahatika kupata watoto wawili mapacha, na watoto hawa walipokuwa wakubwa na kuingia mshuleni, na wao wakavutika na msomo ya sayansi, na  hatimaye maji yakafuata mkondo na wao wakajikuta ni madakitari,….na mmoja wa mabinti hawa, akapata ajira huku Tanzania kama dakitari,
….turejeeni kwanza kwa mwanadada wetu.

Huyu mwanadada tunayemzungumzia, baada ya kumaliza shule, akawa anachukua mafunzo kwenye hiyo kliniki, ni katika kujiendeleza, na pia alivutika na masomo hayo, yeye kwa muda wake wa ziada akawa anafika kwenye hiyo kliniki kupata mafunzo, na kweli akavutika nayo sana, na hata akaona ni vyema, akasomea kabisa mambo ya uzazi , na mataizo yake, na kujikita pia katika mahusiano na matatizo yake.

Ile kliniki ikaamua kumchukua na kumuajiri. Katika masiha lazima kuna kupendana, na huyo binti Ikatokea kupendana na mvulana mmoja huko huko Kenya, walifikia hatua ya uchumba, na mwishowe wakaamua kuoana, na siku wanapeleka posa ikatokea ajali mbaya sana….yule mvulana alipona, lakini alikaa mwaka kitandani, hajiwezi.

Wazazi waile familia hawakurizika na hilo,mila na desturi zetu hazikucheza mbali familia ile ya mwanaume ikaamua kulifuatilia kimila wakakutana na hawa wataalamu wakimila, ambao hawakosi sababu, wakaambiwa huyo binti anamilikiwa na shetani, au kama walivyoliita jinni mahaba, kwahiyo sio rahisi kuolewa, na atakaye muoa atakumbana na matatizo makubwa.

Uchumba ule ukafa, haikuchukua muda akapata mchumba mwingine na huyu walifika hadi hatua ya kufunga ndoa, wakiwa katika hilo tendo la kufungishwa ndoa,yule binti akadondoka, na mara akaanza kuweweseka,na kusema hataki kuolewa kwasababu yeye keshaolewa,…
.
‘Eti nini keshaolewa na nani…..’akaluliza mzazi mmojawapo.

‘Mumesikia wenyewe akisema, keshaolewa na hawezi kuolewa kwa mara ya pili…..’akasema mume mtarajiwa.

NB: Leo nimechelewa kidogo kufika kijiweni, lakini nimeona siku isipite hivi hivi, tupate hicho kipnde kidogo,na nyie huku mkipata nafasi ya kutafakari na kama kuna mwenye maoni au aliwahi kukutana na dhahama kama hiyo changia ili tuboroshe hiki kisa…

WAZO LA LEO: Tujaribu kuwa karibu na watoto wetu, na kila linalotokea kwa watoto, hasa wanapofikia umri wa udadisi, tuwe makini na kauli zetu.  
Na tukumbuke sasa ni dunia ya utandawazi, watoto wetu wanajua mengi ambayo wewe kama mzazi huwezi amini kuwa wanaweza kuyajua, tuwe wadadisi wakuchnguza nyendo na mabdiliko ya watoto wetu, tusipende kuwaachia sana wafanyakazi wa nyumbani,…yote hayo ni majukumu yetu kama wazazi, …tukumbuke kuwa samaki hukunja angali mbichi.


Ni mimi: emu-three

Tuesday, May 29, 2012

Hujafa hujaumbika-43 hitimisho-1




‘ Kila mtu hakuamini ,hata mimi mwenyewe sikuamini hilo, hadi pale nilipopata ushidi wa waza kutoka kwa wahusika wakuu,….maana ilikuwa kama mchezo wa kuigiza, au pwagu na pwaguzi,…mchezo uliochezwa ndani ya famila moja kila mmoja akimtenda mwenzake bila ya mwenzake kujua,….lakini athari zake zikawa zinawaumiza watu wengine ambao….kwa namna moja walikuwa na matatizo kama hayo, wakaingizwa kama ngao …..’akasema wakili mwanadada, huku tukiwa na hamu kila mmoja alikuwa na maswali mengi kichwani ambayo majibu yake tulitarajia kuyapata kutoka kwa huyu wakili mwanadada.

‘Mimi hapo sielewi,matatizo ya familia yanakwenda kuwahusisha watu wengine ….kwa vipi, kama mimi nahusika vipi na matatizo ya familia nyingine, ambayo hata siijui vyema….?’ Nikauliza.

‘Jambo kubwa,ambalo nililigundua ambalo ndilo kiini cha hili tatizo, ni swala la  ndoa na mapenzi, ….’akasema na wote tukabakia tukimwangalia huku tukiwa hatuelewi kabisa nini anachotaka kusema, iweje ndoa na mapenzi yazae vifo vya watu....!
.
‘Ndoa na mapenzi yalete maafa hadi kuuana, kwa vipi na ni nao hawo walisababisha hayo, usiniambia chanzo ni mimi, sikubali kabisa….?’ Nikauliza.

‘Ndoa na mapenzi ni swala nyeti, na tatzio hili limekuwa likiathiri watu bila wenyewe kujua, na hata wanaolisababisha hilo,wanaweza wasijue kuwa chanzo na tatizo ni ndoa yao…..’akatulia na kuniangalia mimi, nikawa kimiya kumskiliza.

‘Bosi anaweza akakorofishana na mkewe huko nyumbani, kwasababu za kindoa, kwasababu za mahusiano ,hasira zile akazipeleka ofisini, na mkamuoana bosi kabadilika, hasira tele, au ukimiya usio wa kawaida au ….hata utendaji mbaya, kiini chake ni ndoa,….hili watu hawajui, na huenda wakataka kujifanya kuwa sio sababu….’akatulia kidogo, na kuinama chini.

Hii ni kuonyesha kuwa wanawake niwatu muhimu sana,…katika jamii, kutokana na wanawake tunaweza kuwa na taifa tulivu na la amani, kwani ndoa ndio chimbuko la kizazi ambacho kinaweza kikawa chema au kibaya, kutokana na malezi, kutokana na masikilizano ya wanandoa, kutokana na sintofahamu inayoweza ikajijenga ndani ya ndoa….’akatulia an kutuangalia …

‘Mimi nazungumzahili baada ya utafiti wa kina, huwezi amini hata viongozi wa nacho wanaathiriwa na hili,…ndio maana watafiti wanapendekeza kuwa ili kiongozi awe bora, lazima nandoa yake iwe bora,…kama ndani ya ndoa yake kunamsuguano, lolote linaweza likatokea…huko kwenye siasa sitaki kupaendea, ila ninalotaka kusema ni kuwa tukio hili, limagubikwa na msuguano, wa ndoa, ….ndoa mbayo iliwakutanisha mafahali wawili, wakawa wanapigana na zinazoumia ni nyasi….’akasema wakili nakutulia.

‘Samahani,….mimi bado umeniacha njia panda….’nikaanza kulalamika.

‘Nilitaka kuwaweka kwazi kuhusu hilo kwanza, kabla sijawaelzea kazi nzimaya hili tukio,…tukio ambalo ni kielelezo kwa jamii, kuwa ndoanimuhimili muhimu katika maisha ya jamii, …tujiribunii kuijua , kuiheshimu, na wanadoa wasikubali tu kuitwa wanandoa, wawe wakiifanyia kazi,….waziboreshe nda zao kwa kujifunza ….kamazilivyo Nyanja nyingine…’akatulia tena kidogo, na mimi nikaoan akma anaipoteze muda nikauliza swali kwa haraka.

‘Tuambie ulivyogundua , maana hadi sasa mimi bado unanichanganya tu, uligunduaje hayo yote maana ukiangalia ilivyo huwezi hata kukisia, wengi walijua kuwa chimbuko la tukio hili zima ni kutoka kwangu, …kwasabbu ya damu yangu moto…..maana kila jambo lililotokea limekuwa likinigusa mimi sio chanzo cha yote, mimi ni kama mhanga mwingine wa ….ndoa za watu wengine.’nikasema na hata mkuu akakubali kwa kichwa huku nikikosa neno sahihi la kumalizia.

‘Dunia hii ina mengi, na binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, kila mara anajaribu kuutumia ubongo wake,  akiona kuwa kuna upenyo wa kuutumia, bila kusahau kuwa na wenzake wana ubongo huo huo na wanafikira hizo hizo,ila pengine kwa njia nyingine….na ndivyo ilivyokuwa kwenye hili tukio zima,….tukio ambalo chanzo chake ni ndoa, hasira zikazaa visasi, na visasi vikawa vinaumiza watu wengine, ambao nao wana matatizo yao kama hayo, na hilo lilipikwa kitaalamu…...’akasema wakili mwanadada akijaribu kutafuta njia ya kutuelewesha maana hadi hapo tulikuwa abado hatujamuelewa vyema , licha ya kuwa mshukiwa wa tukio zima alishajulikana.

‘Ili muelewe hili tukio kwa undani, naona nielezee kwa kupitia wahusika,nikianzia kwako wewe mtoto wa Msomali ,ambaye nitakuita muhusika, ambaye kwa usoni mwa watu ulionekana kama mhusika  mkuu, ….lakini kiundani wewe sio muhusika mkuu, wewe ulikuwa kama tawi kwenye shina,….wapo wahusika wakuu wawili ambao ni shina la tukio zima,…tutakuja kuwajua, ila nataka nianzie kwako wewe ili kukuweka sawa…’akasema wakili mwanadada.

‘Nilishakuhoji sana, na katika kukuhoji huko nilgundua mengi dhidi yako…..mambo haya yanaweza yakaanza mwanzoni tu mwa ndoa, watu hamkai mkaongea, kila mmoja anajiona anajua zaidi ya mwenzake, na likitokea jambo, kila mmoja anakuwa na maamuzi yake,…na hatimye lile pendo linageuka kuwa chuki, wivu, usio na tija,…nakulipizana kisasi,….

Mimi nikakaa kimiya, nikisikiliza ,lakini kwa upande mwingine akili yangu ikawa ikitamani kusikia mengi kwa wkati mmoja, hapo nilikuwa na mawazo ya yule mgonjwa aliyekufa kule hospitalini, nilikuwa nikitaka kwanza aniambie ukweli kuhusu huyo mgonjwa, kabla hajaongea kuhusu mimi, kwahiyo wakati anaanza mimi akili yangu ikazama na kujiuliza,…

Hivi,…..huyo marehemu ...imekuwaje....mbona siambiwi lolote kuhusu yeye, maana kila nilipodadisi lini atazikwa nimekuwa nikipigwa danadana, na kuambiwa hilo nitaambiwa baadaye……na hata ndani ya mahakama sikusiki hakimu akiligusia,….kuna nini kinaendelea,…akili yangu ikasema `hapo kuna kitu nafichwa..na kwanini nifichwe, hata hivyo huyo mtu mbona sijajua umuhimu wake kwangu…’ sikuvumilia nikauliza;

‘Kabla hujaendelea nataka kujua jambo moja,kuhusu huyo marehemu,…..kitu cha ajabu ni kwamba, sijasikia lolote mpaka sasa kuhusu yeye, na maandalizi ya mazishi yake, …., jana nimewauliza mkasema hilo nitaambiwa baadaye, sasa leo naona mnanipiga danadana, kwanza sijamjua ni nani, na kwanini alikuwa akitaka kuongea na mimi, na alitaka kuniambia nini,hamuona mnanitesa mimi kiakili…..’nikalalamika.

‘Ndio maana nawataka mtulie niwape tukio zima , huko kwa huyo anayekutesa akili yako,tutafikia, kwani ni mmoja wa wahusika , sijui tumuiteje , tiutamuita muhusika mashuhuri, kama ulivyo wewe…..maana huyo unayetaka kumjua ni nani, yeye ndiye kiunganishi cha tukio zima, …sasa niwaulize mpo tayari niwaambia nini kilitokea, au bado mna maswali mengine….’akauliza wakili mwanadada na kutuangalia machoni kwazamu, na sisi tulibakia kimiya ….

*********.

 Hiki ni kikao maalumu ambacho tulijikuta tupo mimi, mkuu na wakili mwanadada, hapo tulikuwa  kwenye chumba maalumu cha maongezi, baada ay kutoka kwenye chumba cha  mahakama ambapo tulikutana na hakimu, ambaye alitaka kujua hatima ya kesi inayonikabili mimi, …na baada ya maongezi na hakimu, ilionekana kuwa mimi sina hatia, ila nilishikiliwa ikioanekanna kuwa mimi ndiye muhusika , lakini baada ya uchunguzi , iligundulika kuwa mimi nilitegewa ionekane kuwa ndiye muhusika kiujanaj wa huyo mhalifu, …

‘Sio kwa vile umeambiwa wewe huna makosa ndio uondoke hapa jijini,hapana wewe ni shahidi muhimu sana katika kesi hii, usije ukaondoka, unahitajika sana….’akasema wakili mwanadada.

‘Nimekusikia muheshimiwa ,….’nikasema nakumwanagalia hakimu ambaye alikuwa akimsikiliza wakili mwanadada akiwa anatoa maelezo yake kuhusi kesi niliyokuwa nimekamatwa nayo,…, na alipomaliza kutoa hayo maelezo hakimu akaanza kumhoji wakili mwanadada akuliza swali,

‘Je huyo mshukiwa mumeshamkamata…?’akauliza hilo swali na kumwangalia mkuu, mkuu  ambaye kwa muda mwingi alikuwa kimiya, akionekana mwingi wa mawao akasema;

‘Hajakamatwa muheshimiwa, ila tumeshagundua wapi alipo na mtego umeshawekwa , …nia na lengo letu akamatwe bila umwagaji wa damu…’akasema mkuu.

‘Kwahiyo mnataka kusemaje,maana nimewaita hapa kuwasikiliza nyie,kutokana na kesi zenu ambazo zinakuwa haziishi, kila mnapoleta kesi izenu zinakuwa hazijakamilika, …na hili halinifurahishi, kwanini msitafute ushahidi wa kutosha kabla hamjazifikisha hizo kei zenu kwangu, msifanye kubahatisha, ….hilo sitaki lijirudie tena,mnanielewa…?’akasema muheshimiwa hakimu.

‘Tumekuelewa muheshimiwa, imetokea hivyo kwasababu, kesi hizi zimajisokota , ni watu wajanja walibuni mbinu zao, kwa kuichezea sheria, na saikolojai za watu, wamekuwa wakitumia uzaifu wa wenzao na kujifanya hawahusiki,…na matokeoa yake wakawa wanakamatwa watu wakijulikana wao ndio wahusika, kumbe wahusika wamejificha kiujanja,  na jinsi walivyojipanga isingelikua rahisi kuwajua kuwa ni wao wahalifu,….lakini ubaya hauna kwao wamepatikana…..’akasema wakili mwanadada.

‘Unatakiwa uliweke hilo wazi, na hakikisha kuwa unakuja na ushahid uliokamilika, maana hapa tu umeongea kimafumbo, kitu ambacho sitakitaka kwenye mahakama yangu, uweke uweke kila kitu wazi, ….na hakikisheni kuwa huyo mshukiwa anakamatwa haraka iwezekanavyo, sitaki kusikia matendo macahafuyakitendeka tena, na wakati mumesemamnaushaidi wa kutosha, mkameteni na haki itendeke ,….’akasema muheshimiwa na kuwaangalia  wakili na mkuu kwa kila mmoja kwa wakati wake.

‘Sawa muheshimiwa, leo au kesho utapata taarifa kamili, na tunakuhakikishia kuwa ushahidi wote umekamilika, ndio maana huyo mshukiwa akakimbia,….yeye alichofanya ni kujaribu kuvuta muda ili azima yake ikamilike,  lakini tutahakikisha kuwa hafanyi lolote baya..’akasema mkuu.

‘Sawa hilo tumemaliza, na nini mnataa kusema kuhusu huyu mshukiwa Msomali, maana leo mlisema mtakuja na kauli sahihi, kuwa yeye ndiye mshitakiwa na tunze kusikiliza kesi yake, na kama ndio hivyo ni nani wakili wake, …..?’ akauliza muheshimiwa Hakimu.

‘Kama nilivyosema awali, muheshimiwa, kesi hizi zilijisokota, na hawa watu walikuwa wakitumia mbinu, ambazo zimetufanya tuwakamate watu, tukijua wao ndio wahalafu, kumbe, wao wamejikuta wakiwa kwenye tukioo kama chambo tu, …..’akasema wakili mwanadada.

‘Kwahiyo hapa unataka kusema nini, kuwa kesi dhidi ya Msomali tuifute….nawaonya tena, mjue kwa mtindo huu mnatupoteze amuda wetu, kuna kesi nyingi za kusikiliza, na isiwe kila tukipanga muda wa kesi yenu, mnadai hili halijakamilika na sasa mnadai huyu mshukiwa sio yeye, ni yupi basi mshitakiwa, ili,tuyamalize haya matatizo…?’ akauliza muheshimiwa hakimu akimwangalia wakili Mwanadada, na wakili mwanadada akamgeukiwa mkuu,akiwa anataka yeye aliongelea hilo, na hakimu alipoona wanatupiana macho, akasema;.

‘Kwahiyo mnachotaka kusema hapa ni kuwa kesi dhidi ya Msomali, ifutwe, kwa masharti kuwa, muda wowote atahitajika kama shahidi, ila sasa yupo huru,….sawa?’akasema muheshimwa hakimu na wakili mwanadada akasema;

‘Ndio Muheshimwa, tunaomba kesi hiyo ifutwe dhidi yake,….hana hatia, ila atahitajika kama shahidi…

‘Sawa, mshitakiwa Msomali, kuanzia sasa upo huru,… ila kama ulivyoarifiwa utahitajika kama shahidi, hilo mtaliongelea wenyewe huko, naona hatuna zaidi, …nasubiri mumulete huyo mshitakiwa anayehusika…...’akasema muheshimiwa Hakimu na akawatizama kwa muda wakili na mkuu na alipona wote wapo kimiya akainuka kwenye kiti chake nakuondoka.

Mimi na wakili mwanadada na mkuu, tukatoka na kuingia kwenye chumba cha maongezi, ambapo mimi nilikuwa na mengi ya kujua, na hapo ndipo wakili mwanadada akaanza kuelezea jinsii ilivyokuwa kwenye kisa hiki hatua kwa hatua…..akianzia kwangu,na malezo yake yalijifanya nijijue …. na hapo akili yangu ikama kama mtu aliyezibuliwa,,…ni kama mtu aliyekuwa kaingiwa na maji masikioni, na yale maji yakatolewa……

NB: Haya wapenzi wa blog hii, naanza hitimisho la hiki kisa…..zipo njia nyingi za kuandika visambalimbali,  unaweza ukaandika kisa ukikianzia kwenye shina au aukakianzia mwishoni,ukakianzia kwenye  matawi yake,….kisa hiki ni mtindo mwingine ambao tumeaniza  kwenye matawi, na sasa tunaingia kwenye shina…mpo hapo…
WAZO LA LEO: Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora ni maisha ya mume na mke ndani ya ndoa. Na  ili starehe hiyo ikamilike na kuleta matunda bora na mema, matunda ambayo nikiini cha amani na upendo duniani, ni bora wewe unayatarajia kuingia kwenye ndoa ukatafuta mke au mume mwema, na pia ni muhimu ukaijua ndoa na misingi yake vyema.  

Ni mimi: emu-three

Monday, May 28, 2012

Hujafa hujaumbika-42



Niliambiwa kuwa nahitajika kwenda kumuoma mgonjwa kwani keshazindukana na anahitaji kuniona mimi, nikajiandaa kwa haraka, na moja kwa moja nikachujuliwa kwenye gari , hadi huko hospitalini, na tulipofika tulikuta walinzi, yule dereva aliyenichukua akajitambusliha na kuonyesha ushahidi wa maandishi kuwa kweli ni yeye, ilikuwa ni utaratibu, lakini wanamjau kuwa ni mmoja wa dereva wao, tukaruhusiwa kupita baada ya mimi kukaguliwa mwili mzima kuwa sina silaha yoyote.

Nikaingizwa kwenye chumba cha maalumu cha wagonjwa mahututi, na pale nikamuona mgonjwa akiwa kalala mipira yote inayohitajika ikiwa imewekwa mwilini mwake, nikasogea na kusimama mbele yake, alikuwa kafumba macho, baadaye akayafumbua na kuniangalia, …kwanza aliniangalia kwa makini, halafu kama anatoa mshangao, akasema;

‘Sasa hivi sitaki kuongea na wewe, bado najisikia vibaya, ngoja nipumzike kidogo, nitakuona baadaye…usiondoke mbali…’akafumba macho na mimi nikabakia nimeshangaa, maana niliambiwa kuwa huyo mgonjwa anataka kuongea na mimi, lakini yeye mwenyewe anasema bado hajisikii vyema.

Nilisimama pale kwa muda mara akaja askari na kuniuliza kuwa mgonjwa kasema nini, nikamwambia, mgonjwa kazungumza kwa sauti ya shida akasema anajisikia bado anajiskia vibaya, anahitaji kupumzika kidogo, ataongea na mimi baadaye, kwahiyo nisubiri,nisiende mbali….

Basi yule mlinzi akaniambia nikakae pembeni, kuna sehemu wanapokaa madakitari, nikaambiwa nikae hapo nisubiri, ni chumba kidogo,ila unaweza kuona kule kitandani.

Nilikaa pale kwa muda mrefu hadi usingizi ukanipitia, na mara nikazindukana, ….sijui ilikuwaje ,ila nilipofumbua macho, niliangalia moja kwa moja  kule kwenye kitanda alipolala mgonjwa, nikaona daktari kamuinamai mgonjwa,…akawa kama anamwangalia , akasimama na  kuchunguza ile mipra iliyokwenda hadi kwenye mashine, akasogea hadi kwenyemipira mmojawapo akaukata na mkasi…

Nikashangaa, …akasoge kwa nyuma na kusubiri kidogo,  akamwangalia mgonjwa, ambaye alikuwa kama anatingishwa, akasoegea pembeni na mara akasogelea ile mashine ambyo mwanzoni kwa umbali ule ilikuwa ikionyesha ile mistari ya kupanda na kushuka sasa ikawa imenyooka, na ikawa inapiga kelele, akasogea mbali na akageuka akawa anakuja pale nilipokuwa nimekaa, moyo ukaanza kunidunda,…

Alikuja hadi pale nilipokaa, kwa jinsi nilivyokuwa nimekaa pembeni, hakuniona kwa haraka, alichofanya ni kuvua ile miwani yake, akawa kama anaipangusa na kitambaa, halafu akageuka,  akaniona, alishituka, lakini akajifanya kama vile hajashituka, aliniangalia kwa muda bila kusema kitu.Mimi kwa kiherehere change nikamuuliza;

‘Docta vipi,mbona umeukata ule mpira wa mgonjwa huoni kuwa ndiyo inayomsadiai kupumua…?’ nikamuuliza.

Hakusema kitu, akageuka kutaka  na kunitizama, huku akiwa kava miwani, akasema ;

‘Mgonjwa alishapona, hahitaji ile mipira anampa shida….na hayakuhusu wewe,….’akaondoka hadi mlangoni, alipofika pale mlangoni, akaataka kamakurudi, lakini alihisi kuna matu anakuja, akageuka nakuondoka kwa haraka.Mimi bila kupoteza muda nikaenda pale alipolala mgonjwa nikamwangalia, nilikuta katulia kimiya, huku macho yamemtoka..

Nikarudi pale nilipokuwa nimekaa, nikaona sehemu ya simu ya kuita dakitari nikapiga haraka, na mara dakitari akaja ;

‘Mbona kaja dakitari hapa na kukata ule mpira kwa mgonjwa,….?’ Nikauliza.

‘Eti nini….!, dakitari, dakitari gani huyo….?’ Yule dakitari akashangaa, akaenda pale alipo yule mgonjwa, na kuangalia, akakuta ule mpira kweli umekatwa, akachukua simu yake na kupiga namba,mara wakaja watu wanne, wakachunguza na baadaye , wakamfunua yule mgonjwa….

Yule dakitari wa mwanzo akaongea na mwenzake, na yule mwenzake akaja pale nilipo na kuniambia nitoke mle ndani niende nje, maana wapo kazini,….nikasita , kwani nilitaka kujua nini kinaendelea, lakini yule dakitari akawa kanishika mkono na kunivutia nje,… nikatoka, na nilipofika mlangoni nikageuka kuangalia kule kitandani, nikashangaa, na kabla sijaweza kuangalia vyema,… yule daktari akafunga mlango haraka, nikabakia pale mlangoni, nikiwaza, ni kweli nilivyoona au nimacho yangu tu, yanajenga hisia.

*******
Nilipotoka pale hospitalini, sikurudishwa kule kwenye mahabusu, nilipelekwa nyumbani kwa Mkuu, waliniambia wanafanya hivyo kwa ajili ya usalama wangu. Nilipouliza ni nani anataka kunizuru, wakasema hawataniambia hilo kwa sasa.

Nikafika kwa Mkuu, nilikuta ulinzi mkali, nikaonyeshwa chumba ambacho natakiwa nikae, kama mahabusu, nilijiona huru kidogo, ingawaje niliitwa mahabusu, nikaonyeshwa kazi ambazo natakiwa kufanya kila siku, kuhudumia bustani na kazi ndogo ndogo za hapa na pale.

Kesho yake nilichukuliwa na kwenda kule hospitalini, nikaambiwa kuna gwaride la utambusho , natakiwa kumtambua huyo docta niliyemuona akiukata ule mpira kwa yule mgonjwa.

‘Ukimuona utaweza kumkumbuka…?’ akaniuliza askari mpelelezi.

‘Ninaweza maana alivua miwani nikamuona vyema usoni…’nikasema.

‘Hakikisha kuwa unamkumbuka vyema, ni muhimu sana…’akasema huyo mpelelezi,

Basi gwaride hilo la utambulisho , likafanyika, lakini sikuweza kumtambua huyo dakitari, hakuwepo kabisa, na wakasema zoezo hilo limekamilika, nikaambiwa nirudi huko nilipokuwa. Zikapita siku mbili, na ya tatu, wakaniambia kuwa nimekubaliwa kupewa dhamana, lakini sitakiwi kusaafiri au kwenda mbali ya hili jiji. Nikashukuru sana angalau nipo huru, licha ya kuwa nipo kwenye uchunguzi .

 Siku hiyo nikiwa nyumbani kwangu wakanijia wageni , alikuwepo mkuu, mwanadada mpelelezi na mkuu, walisema kuwa walikuja kwangu kuna mambo wanataka kuyaweka sawa, wanahitaji  kunihoji maana kesi imeshakamilika na kesho yake itakuwa siku ya kuipeleka mahakamani, ninaweza nikahitajika. Nikasema haina shida.

Wakili mwanadada na mkuu, wakakaa kwenye kiti, lakini wakili mkuu, yeye alikuw akasimama, akiangalai nje, kwakupitia drishani,nilimuona kama ana harakaya kutaka kuondoka, kinyume na wenzake, wakisema kuwa hawahitaji muda wangu mwingi ni maswali machache ya hapa na pale.

Aliyeanza kuniuliza maswali ni mwanadada wakili, akaniuliza , naweza kumuelezaje yule docta aliyefika siku ile kule hospitalini. Nikawaelezea jinsi anavyoonekana, na niliwatizama wote kuangalia kuwa nani mwenye umbile sawa nay eye, sikuweza kumlinganisha na yoyote, ila nikaona kama anakaribiana na …, nikasema.

‘Umbo lake linakaribiana sawa kidogo kama huyo wakili wenu mkuu…’nikasema na yule wakili mkuu akageuza kichwa na kuniangalia mra moja, halafu akawa akageukia huko alipokuwa akiangalia, na baadaye akauliza swali bila ya kuniangalai aaksema.

‘Una uhakika na hilo…maana ni muhimu sana kwetu…?’akaniuliza huyo wakili mkuu.

‘Nimesema kiumbile wanakaribiana, sina uhakika zaidi ya hilo…’nikasema.

Waliniuliza maswali mengine, na baadaye waliporizika wakaondoka, na siku inayofuata akaja wakili mwanadada, na tukawa tunaongea mambo mengi, baadaye akaniuliza swali ambala waliniuliza jana yake.
‘Una uhakika ukimuona huyo docta hata leo unaweza kumkumbuka vyema..?’ akauliza.

‘Kwanini nisimkumbuke, sura yake haijanitoka, lakini kuna jambo nataka nikuulize kwanza’nikasema.

‘Uliza….unataka kuuliza kuhusu nini, uliza tu,…?’ akasema na kuniangalia kwamashaka huku akijaribu kutoa tabasamu,licha ya kuonekana kukerwa, hakuwa na uso wa furaha, nikajua labdani kwasababu ya kazi nyingi.

‘Mna uhakika kweli kuwa yule mgonjwa kafariki ?’ nikauliza,na yeye akawa kama kashituka na kuniangalai bila kunjibu kwa muda akasema;

‘Kama mgonjwa alikuwa akipumulia mshine, na ile mashine ikaondolewa mipira kabla hajazindukana anaweza akapona…wewe mweyewe unakiri kuwa ulipoingia ulimkuta kakodoa macho kuonyesha kuwa uhai haukuwepo….hukumgusa,kuhakikisha ?’ akaniuliza.

‘Sikumgusa, na kweli kama mtu alikuwa akipumulia mashine,ikiondolewa, sizani kama anaweza kupona, na kweli nilipofika pale niliona ile mishale ya kuonyesha uhai ilikuwa imesimama, na hata mgonjwa  mwenyewe alionyesha kabisa kafariki, maana alikuwa katoa macho….lakini…’nikasema.

‘Lakini nini tena….usihisi vitu kama hivyo, unachotakiwa ni kusema ulichokiona,sio kuhisi,…..nikuulize swali,kwanini unamashaka, na kwanini ukaniuliza hilo swali?’akauliza wakili mwanadada, nikawaza kwa muda, nikashindwa la kuongea, maana hisia zangu siku ile zilinisuta, nilikuwa na uhakika kabisa, kuwa yule mgonjwa alikuwa kafariki, ingwaje sikumgusa, lakini wakati natoka pale mlamngoni niligeuka nakaona kama yule mgonjwa alikuwa kaka kitandani akiongea na wale madakitari, …huenda ni hisia zangu tu,…sikusema kitu tena.

‘Una mshaka gani..?’akaniuliza tena wakili mwanadada.

‘Hapana, maana hisia zangu zinanituma kama huyo mgonjwa,……hapana, unajau mimi ninakuw ana mahisia ya ajabu,huenda ni kuchanganyikwia tu, ila natamani nimuone huyo…hayo maiti kwa kwanza ili nihakikishe mwenyewe…..’nikasema.

‘Ina maana unataka ukaikague hiyo maiti yake uhakikishe  kuwa kafa,kama unahitaji hivyo ninaweza kukufanyia huo mpango, haina shaka,….’akasema wakili mwanadada.

‘Hapana….  sio hivyo, ..haina haja, kama wewe umethibitisha hilo, haina haja….’nikasema na kutulia kimiya, na baadaye huyo wakili mwanadada akaondoka,na kuniambia niwe mwangalifu katika majibu yangu, na pia niwe mwangalifu kiusalama, nisiondoke ondoke sehemu yoyote bila kutoa taarifa. Nikasema nitafanya hivyo.

 Ilikuwa usiku wa saa sita hivi, nikiwa nimechoka sana,nilipata kibaraua sehemu, na nilifanay hiyo kazi hadi saa kumi, nilipotoka hapo nikaenda sehemu nikapata chakula ambacho nilikichukuliwa kama mla wa siku, na kurudi nyumbani kwangu, sikutaka kutembea sehemu nyingine yoyote maana nilishakanywa kuwa kuna watu wanataka kuniua.

 Ilipofika saa sita za usiku, nikasikia mtu anagonga mlango, nikashituka, kwanza niliogopa kabisa kumfungulia, lakini alipoondelea kugonga, ikabidi nimuulizekuwa yeye ni nani...

‘Mimi ni askari usalama usiwe na wasiwasi….’akasema huyo mtu, nikafungua mlango kwa mashaka.

‘Mbona unaniamusha mudakaam huu ,kuna tatizo …?’ nikamuuliza.

‘Kwasababu ni muhimu sana, na nimetoka kufuatilia mambo fulani kuhusu hii,kesi, na nimeona kabla sijalala niwe na uhakika na jambo moja dogo tu, usijali,na samahani kwa kukusumbua, najua unanikumbuka…’akasema , aliposema `unanikumbuka'  nikamwangalia, sikuwa nimemwangalia vyema mwanzoni,baada ya kusema yeye ni askari usalama,nilishaju labda ni mmoja wa hawo walinzi niliowaona hapo nje.

‘Lakini muda kama huu, jamani…aaah, ni wewe tena, mimi nilijua tumemaliza mchana,…’nikalalamika.

‘Hatuna muda maalumu kwetu, tukihitaji jambo au tukigundua jambo, lazima tulifuatilie, na mimi nimegundua kitu, unajue pale tkupokuja mchana kukuhoji ulinitia mashaka kidogo, angalia yako kwangu ilinitia mashaka, ndio maana nimekuja kukuuliza vyema, nataka kuhitimisha taarifa yangu….’akasema.

‘Sawa lakini nilisema wewe unafanana na huyo docta kimaumbile, sio kabisa kabisa,….’nikasema na muda huo tukawa tumetizamana uso kwa uso, na mwanga toka dirishani ukawa uammulika usoni, na kwamuda huo alikuwa hajavaa miwani, akili yangu ikagundua kitu, sikuwahi kutizamana naye uso kwa uso jana yake,…,laini sasa tulipoangaliana nikakumbuka na mwili ukaanza kunisisimuka,a…..kilichoniponza ni kutokuwa mvumilivu, nikamuuliza swali;

‘Kuna ndugu yako ni docta…?’ nikamuuliza.

‘Kwanini unaniuliza hivyo…?’ akasema.

‘Kwasababu nahisi kama unafanana na yule docta,  nakumbuka kabisa yule docta alipovua ile miwani, mnaonekana kufanana naye kabisa hata sura….’nikasema.

‘Una uhakika na hilo,..? ‘ akaniuliza kwa sauti kali kidogo, halafu akailegeza na kusema

‘Ndilo maana nimekuja kukuona tena, nilitaka kujua kuwa kweli unakumbuka vyema,…usiwe unahisi , uwe na uhakika na hilo uliloliona, ukihisi na kuongea kitu ambacho huna uhakika nacho utaenda jela,..mimi sio docta, na walsinandugu docta, chunga sana mdomo wako,…’akasema na kutabasamu.

‘Una maana gani kusema hivyo,….kwani,ni…mbona… ?’nikakawa nimeshikwa na kigugumizi, na akawa kama anataka kuondoka akasema;

‘Kwasabbu kesi itaanza kesho na wewe unatakiwa twende ukawaangalia mdakitari wote tena kuhakikisha hilo, ili kama unaweza kumkumbuka huyo dakitari uliyemuona…..inawezekaan siku ile hukuwa makini katika utambuslho ule, ….’akasema huyo wakili.

‘Lakini kazi hiyo nilishaifanya, na sikuweza kumuona docta yoyote anayefanana na huyo niliyemuona…labda kama kuna mwingine kaongezeka..’nikasema.

‘Haina shaka, ….tutaona hapo kesho, tukijaliwa,….hata hivyo naona kuna kitu kinafanyika nyuma ya mgongo wangu, tusubiri hiyo kesho, tutaona mwisho wake….na nakukuanya tena, usiwe unajibu kutokana na hisia zako,…ukijifanya mjanja uanongea saana, utajiponza…..haya lala salama na omba sanamungu wako…..’akasema na kuanza kuondoka na mimi nikaongea kujikosha,hasa palenilipomuona kuwa amekasirika.

‘Mimi ….nilisema kuhisi na kulinganisha tu muheshimiwa, sikuwa na maana mbaya kwako wewe muheshimiwa, nilipewa hicho kibali cha kumuona huyo mgonjwa, tu, mengine yaliyotokea mimi sikujua kuw ayatatokea, na sio kuwa ni wewe niliyekuona…, nafafanisha tu muheshimiwa niwie radhi,kama nimekosea, nitachunga mdomo wangu…’nikasema.

‘Haina shida….’akasema na kuondoka.

Alipoondoka yule wakili nikapokea simu, kutoka kwa wakili mwanadada, akaniuliza kuwa nilitembelewa na nani, nikamwambia, akasema amekuja baada ya kusikia kauli yangu kuwa huyo docta niliyemuona anafanana na huyo wakili, aliamua kuja kuthibitisha kumbukumbu zangu kuwa una uhakika na hilo ulilolisema,….’akasema.

‘Lakini swali mliloniuliza lilitaka nilinganishe na umbile, `anafananaje', ningejibuje bila kulinganisha na kitu ninachokiona,kosa langu hapo lipo wapi…..?’ nikauliza.

‘Ndio maana nahitaji uwe makini katika majibu yako, sema kile ulichokiona usijibu unavyohisi,,…sawa..kama kuna lolote bonyeza simu yako pale nilipokuonyesha,na hakikisha humfungulia  mtu mlango kwa hivi sasa uwe makini, …

‘Lakini nakumbuka mlisema kuwa kuna walinzi wananilinda, nanimeona walinzi hapo nje wakiwana silaha,….’nikasema

‘Ndio wapo walinzi, lakini huwezi jua, ukio na mashaka, tumia akili yako, usiwategemee sana,, ….’akasema na kukata simu.

Sikuweza kupata usingizi, nilihakikisha kuwa nimefunga mlango vyema , kitanda changu kipo eneo la dirishani, hapo ikanitia wasiwasi, nilichofanya ni kuweka mito, mfano wa mtu aliyelala, nikahukua kigodoro kidogo, na kujilaza chini ya meza yangu kubwa, ….hayo niliyafanay kutokana na zile hisia zangu zinavyonijia.

Nilizindukana toka kwenye usingizi, ilikuwa kama saa tisa hivi, nikahisi dirisha likiguswa, na mara nyavu za dirisha zikakatwa, sikusogea pale nilipo, niliinua kichwa kwa mashakanakutizamadirishani ….nikasubiri.

Kwanza nilihisi labda ni wezi, lakini mbona nimeambiwa kuwa kuna walinzi wananilinda kwa nje,nikasubiri…
Mara nikaona kitu kikijitokeza, ni kurunzi ndogo,ikawainamulikapalekitandani, na mara  kikatokeza kitu kingine, ….moja kwa moja nikajua ni sehemu ya mbele ya bastola, ikaelekezwa  pale kitandani,…ambapo nalala, risasa zikafyatuliwa tatu mfululizo,…..tufu-tufu tufu…., lakini hiyo bastola haikutoa sautii, nafikiri walikuwa wameweka kitu cha kuzuia risasi, na baadaye kimiya kikatanda.

Haikupita muda akaja, wakili mwanadada, akagonga mlango na kujitambuslisha, na mimi nikamfungulia, akaniangalia usoni kwa mashaka na kuniuliza nini kimtokea, nikamhadithia akasema anahisi kati ya walinzi kuna ambao sio waaminifu, hajajua ni nani, lakini hilo watalimaza leo hii.

‘Kwa vipi….?’ Nikauliza.

‘Tumeona tukizidi kuvumilia mambo yatazidi kuwa mabaya, na uhai wako utakuwa hatarini, tuna ushahidi wa kutosha kwa sasa, na huyo aliyekuja kwako na kukata nyavu za dirisha alikuwa akifuatiliwa kwa karibu, nashindwa alifikaje na kufanya hivyo, wakati wapo walinzi hapo nje….’akasema wakili mwanadada.

‘Kwani ni nani huyo….?’ Nikauliza huku nikiwaza mengi yaliyotokea, na wakili mwanadada akaniangalia kwa makini, na kabla haongea kitu, mara mlango ukagongwa na aliyeingia alikuwa mkuu, na yeye akanitizama kwa uso wa wasi wasi, akaniuliza.

‘Vipi upo salama….?’ Akauliza.

‘Nalijua mlitajia mtaikuta maiti, au sio,..lakini kama unavyoona mkuu nipo salama…ila mpaka sasa siamini kuwa nipo hai, …hapa nilipo mwili mzima unatetemeka..’nikasema na mkuu akamgeukia wakili mwanadada nakusema;

‘Usituelewe vibaya kabisa, ….’akasema na na bila kuongeza neno akamgeukiwa wakili mwanadada na kusema;

‘Mtu wetu katoweka,…..’akasema.

‘Unasema nini mkuu….toka muda gani, mbona sielewi, mambo mengi yanatendeeka sivyo kinyumena tulivyopanga,….atakuwa kaendawapi huyu mtu?’ Akauliza kwa huku akiwa katoa macho ya kushangaa..

‘Nahisi keshagundua kuwa yupo matatani, …maana kulipopambazuka tu, akawa haonekani, na simu zake zote hazipatikani, na mkewe anasema hajui mumewe aliondoka muda gani, na hajui wapi alipokwenda, maana jana yake walikorofishana, na kila mmoja alilala kivyake,….’akasema mkuu.

‘Ina maana wanalala chumba tofauti….?’akauliza waliki mwanadada.

‘Wana chumba cha akiba, huwa wakikorofishana mmojawapo  anakwenda kulala kwenye hicho chumba chao cha akiba, kwahiyo yeye hakuona ajabu alipoamuka na kumkuta mumewe hayupo, ndivyo wanavyoishi, ….ila kilichomtia mashaka ni kuona kuwa abadhi ya nguo hazipo, na moja ya sanduku la kusafiria halipo, kuonyesha kuwa huyo mtu kaondoka safari….’akasema mkuu.

‘Na huyo mkewe yupo wapi kwa muda huu..?’ akauliza.

‘Kashikiliwa kituoni, tunaona njia peke ya kumnasa huyu mtu ni kumshikilia mkewe…..’akasema mkuu.

‘Hapana msifanye hivyo, muachieni na inatakiwe iwe kama hakuna mtu anayemfuatilia, tutamnasa tu, sizani kama katoka nje ya hili jiji,atakuwa kajificha kwenye moja ya nyumba zake ndogo, wasambaze vijana wako waaminifu….’akasema wakili mwanadads.

‘Hilolimeshafanyika, na ….kweli tumamuachia huyo mke wake, alikuwa nahitaji muongee na yeye,anasemani muhimu sana….’akasema mkuu.

‘Sasa kazi imeanza,ni muda wakuwa waangalifu kuliko sikunyingine zote, na ulinzi mkali unahitajika, na tunahitaji watu watu wanaoaminika, …kutoweka kwa huyu jamaa kunatuweka kwenye mashaka makubwa, sijui ana mipango gani, …hapa naingiwa na mashaka kuwa lolote baya linaweza likatokea…’akasema na kumgeukiwa wakili mwanadada na kuendelea kuongea kwa kusema;

‘Nashauri, tumuondoe huyu mtu hapa haraka, ….ni bora aje akakae kwangu…’akasema mkuu na kabala hajaendelea kuongea nikasema kwa haraka;.

‘Hapana mimi siendi popote, ….hisia zangu hazimwamini mtu yoyote tena, naona nitajilinda mwenyewe kuanzia sasa, maana lililotokea usiku wa leo, limenipa fundisho,nitajua wapi pa kwenda na jinsi gani nitajilinda, nahisi sina usalaam tena, nikiwategeema nyie….’nikasema huku nikiwa na mawazo mengi.

‘Usijali upo kwenye ulinzi, yote yanayofanyika yanafuatiliwa kwa karibu….huo ulikuwa mtego…ila…’akasema wakili mwanadada nakumwangalia mkuu, akitaka kusema kitu.

‘Niwaulize kama nisingelikuwa na wazo hilo la kujificha , na kuweka mito kama mtu aliyelala, ningekuwa wapi saa hizi,….kama ni ulinzi wa namna hiyo wa kiniweka mimi kama chambo, sikubali tena, nimechoka na matatizo,…..’nikasema na wakili mwanadada akniangalia akionyesha uso wa kutahayari, akageuka kumwangalia, alitaka kusema kitu, lakini mkuu akawahi nakusema.

‘Mungu yupo pamoja na wewe, tunakubali kuwa kuna kosa limefanyika, na hilo tumeshalisawazisha, mengine ni mambo ya ndani,kama yupo mtu nyuma ya hili tutamshughulikia, na hilo tunalifuatilia kwa karibu….ujue kila kitu hutokea ili iwe ni sababu …na hata kama tungeliweka ulinzi wanamna gani,kama lilipangwa kutokea lingelitokea tu,…hapa tuliweka watu, tukijua hakuna mtu atakayefika kwako, lakini wamefika….nahisi kuna mtu anatusaliti….’akasema mkuu huku akikwepa kuniangalia machoni.

‘Kwamtaji huo, mimi nitajilinda mwenyewe, sihitaji ulinzi wenu tena, kwani nimegundua kuwa kil nikIutegemea ulinzi wenu, nijikuta naingia kwenye matatizo, angalia kama leo, kama nisingejihami mwenyewe, nini ingetokea,,….’nikasema na wote wakaniangalia huku wametahayari usoni.

NB: Tunakuja sasa kwenye hitimisho, ambapo maswali mengi yaliyokuwa ymejificha yatagundulikana, nii nanii huyo yupo yuma ya haya yote, je mgonjwa aliyekufa ni nani, na kwanini hisia za msimuliaji zinasema `hajafa' hayo namengine mengi tutakuja kuyaona. Tupo pamoja

WAZO LA LEO: Tujaribu sana kuchunga ndimi zetu hasa pale tunapohisi jambo bila kuwa na ushahidi nalo, Unaweza ukongea jambo kwa nia njema tu, kumbe ile kauli ikatafsiriwa vibaya,na matokeo yake ikaleta dhahama, kwahiyo ni bora kukaa  kimiya kama huna ushahidi kuliko kuongea kutokana na hisia zako ukazusha mikangano isiyo ya lazima. kama walivyosema wahenga,bora nusu shari kuliko shari kamili. 

Ni mimi: emu-three

Search This Blog

Loading...